1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Afrika Kusini kukabidhiwa ripoti ya kupanga matokeo ya mechi

11 Aprili 2015

Waziri wa michezo wa Afrika Kusini anasema amepokea hakikisho kutoka kwa kamati ya maadili ya FIFA kuwa itakamilisha na kuwasilisha ripoti mwezi Juni kuhusiana na madai ya kupangwa matokeo ya mechi

https://p.dw.com/p/1F6Ma
Freundschaftsspiel Brasilien Südafrika Fußball
Picha: Marco Longari/AFP/Getty Images

Matokeo ya mechi yaliyadaiwa kupangwa kabla ya dimba la Kombe la Dunia mwaka wa 2010.

Fikile Mbalula amesema alikutana na mwenyekiti wa jopo la upelelezi la kamati ya maadili, Cornel Borbely, mjini Zurich wiki hii ili kufafanua kuhusu hali ya ripoti hiyo iliyosubiriwa kwa muda mrefu.

FIFA ilisema mwaka wa 2011 kuwa ilikuwa na ushaidi wa kutosha kuwa baadhi ya mechi za maandalizi za Afrika kusini zilizochezwa katika wiki za kabla ya Kombe la Dunia zilipangiwa matokeo. Hakuna wachezaji waliotuhumiwa, lakini marefarii walishukiwa kushirikiana na mpangaji matokeo ya mechi aliyehukumiwa Wilson Raj Perumal na kuvuruga matokeo ya michuano.

Mwandishi: Bruce Amani/AFP/Reuters
Mhariri: Mohamed Dahman