Miongoni mwa matukio ya Afrika ambayo yameangaziwa kwenye magazeti ya Ujerumani wiki hii ni pamoja na maandamano yaliyomlazimisha rais wa Algeria Abdelaziz Bouteflika kuachana na mpango wake wa kuwania urais kwa muhula wa tano, juhudi za kupambana na ujangili Afrika na hatua ya nia njema ambayo Ujerumani inakusudia kuchukua ili kuendeleza uhusiano mwema na koloni lake la zamani Namibia.