Maelfu ya wakatoliki wamemuaga aliyekuwa kiiongozi mkuu wa kanisa hilo Papa mstaafu Benedict wa 16 huko Vatican aliyefariki Jumamosi akiwa na umri wa miaka 95. Maelfu ya waumini walianza kupanga foleni tangu alfajiri kuutazama mwili wa Papa Benedict wa 16. Saumu Mwasimba alizungumza na Askofu Methodius Kilaini wa kanisa katoliki huko Tanzania na alikuwa na haya ya kusema.