Afisa wa UAE kuzuru Qatar
5 Desemba 2022Kiongozi wa Umoja wa Falme za Kiarabu Sheikh Mohammed bin Zayed Al Nahyan, amefanya ziara ya kushtukiza nchini Qatar leo, ikiwa ni ya kwanza tangu alipoongoza hatua ya mataifa manne ya kiarabu ya kuisusa Qatar kidiplomasia kwa zaidi ya miaka mitatu.
Shirika la habari la serikali la WAM, limeripoti kuwa sheikh Muhammad ambaye pia ndiye mtawala wa Abu Dhabi anaitembelea Qatar kwa mwaliko wa kiongozi wa nchi hiyo ya Ghuba, Sheikh Tamim bin Hamad Al Thani.
Sheikh Mohammad alizingatiwa na wachambuzi kuwa moja ya vinara wakuu wa kuisusa Qatar kidiplomasia kuanzia mwaka 2017, uamuzi uliozusha mzozo mkubwa wa kisiasa kwenye ulimwengu wa kiarabu.
Ususiaji huo uliozijumuisha pia Bahrain, Saudi Arabia na Misri ulihusisha kuzuiwa kwa njia za usafiri wa angani na baharini. Mvutano huo ulimalizika Januari 2021 muda mfupi kabla ya rais Joe Biden kuchukua madaraka nchini Marekani.