1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Afisa wa FIFA aadhibiwa kwa kuvunja sheria

8 Julai 2015

Afisa mmoja mkuu wa shirikisho la kandanda duniani, FIFA aliyesimamia jopo la kutathmini utoaji vibali vya kuandaa kombe la dunia la mwaka wa 2018 na 2022 amepigwa marufuku ya miaka 7

https://p.dw.com/p/1Fups
Chile ehemaliger chilenischer Verbandspräsident Harold Mayne-Nicholls
Picha: picture-alliance/AP Photo/L. Hidalgo

Taarifa ya FIFA imesema Harold Mayne-Nicholls, mwenye umri wa miaka 54 hataruhusiwa kushiriki maswala yeyote yanayohusiana na kandanda kwa kipindi cha miaka saba ijayo.

Kamati ya maadili ya FIFA imesema kuwa itatangaza wazi madai dhidi yake mara baada ya hatu hiyo ya kumpiga marufuku itakapoaanza kutekelezwa.

Mayne-Nicholls anahoji kwa nini kauli hiyo imechukuliwa na kutangazwa wakati ambao FIFA inafahamu wazi kuwa anaendelea kukata rufaa

Mayne-Nicholls aliyekuwa wakati mmoja mwenyekiti wa shirikisho la soka la Chile alitajwa miongoni mwa watu 5 ambao kamati ya maadili ya FIFA ilkuwa imeanzisha uchunguzi dhidi yao

Alikiri wakati wa uchunguzi kufanya mazungumzo ya kibinafsi na wakuu wa shirikisho la soka la Qatar akitaka jamaa wake waajiriwe katika chuo cha mafunzo ya kandanda cha Aspire.

Mwandishi: Bruce Amani/Reuters
Mhariri: Caro Robi