Afghanistan
23 Agosti 2008Kabul:
Vikosi vya nchi shirika vinavyoongozwa na Marekani nchini Afghanistan, vimeamua uchunguzi ufanywe baada ya wizara ya mambo ya ndani ya Afghanistan kusema hujuma za mabomu za vikosi shirika zimegharimu maisha ya raia 76 magharibi ya nchi hiyo.Rais Hamid Karzai amelaani kile alichokiita "kifo cha mashahidi zaidi ya 70,wengi wao wakiwa wakiwa wakinamama na watoto."Viokosi vya nchi shirika vinavyoongozwa na Marekani vilisema jana waasi 30 wameuliwa akufuatia mapigano pamoja na vikosi vya usalama vya Afghanistan na vikosi vya kimataifa vikisaidiwa na helikopta za kivita katika mkoa wa Shindand.Serikali ya Marekani pia inatilia shaka taarifa ya serikali ya Kaboul."Tuhuma zote kuhusu kuuliwa raia wasiokua na hatia zitachunguzwa kwa makini.Vikosi vya nchi shirika vinafanya kila liwezekanalo kuwaepushia hasara ya maisha raia.Uchunguzi utafanywa."Taarifa ya vikolsi hivyo vya kimataifa imesema hii leo.Maandamano yameitishwa kulaani mauwaji hayo huko Shindand.Waandamanaji wamebeba mabango dhidi ya rais Hamid Karzai na dhidi ya kuwepo vikosi vya nchi shirika nchini humo.