1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Afghanistan na Ujerumani

1 Juni 2009

Ujerumani yamteua mjumbe maalumu kwa Afghanistan na Pakistan

https://p.dw.com/p/I1Ya

Mchafuko wa hali ya kisiasa nchini Afghanistan, unazidi mno.Kutumika kwa majeshi ya Ujerumani huko kuna shabaha ya kuiimarisha Afghanistan inayojikuta katika hali ngumu kabisa.Kwa kumteua Bw.Bernd Mutzelburg, mjumbe maalumu wa wizara ya nje ya Ujerumani kwa Afghanistan na Pakistan,ni azma ya serikali ya Ujerumani kutilia nguvu juhudi zake za kibalozi katika eneo hilo.

Mkakati mpya wa serikali ya Marekani juu ya Afghanistan,unasisitiza umuhimu mkubwa wa jirani Pakistan katika kuutatua mgogoro wa Afghanistan.Kutokana na mkakati huo, serikali ya Marekani imemteua Bw.Richard Holbrooke mjumbe wake maalumu tangu kwa Afghanistan hata kwa Pakistan.

Mjumbe huyu wa Ujerumani kwa nchi hizo mbili,Bernd Mutzelburg, ni mshirika wa moja kwa moja wa mazungumzo wa Bw.Holbrooke.Wajumbe wote hao wawili, wametwikwa jukumu la kuimarisha juhudi za kidiplomasia zenye kulenga kuiimarisha Afghanistan.Bernd Mutzelburg,ameueleza mkakati wa Ujerumani kwa Afghanistan ni kuchangia kuijenga Afghanistan upande wa kiraia kwa kujumuisha ulinzi wa kijeshi.

"Nadhani,hiyo ndio iliokuwa shabaha ya mchango wa Ujerumani huko Afghanistan wakati wote kuona jeshi lake linachangia juhudi za kuijenga mpya nchi hii.Tunaelewa kuwa,maendeleo yaweza tu kupatikana katika hali ya usalama .Na hilo ndilo jukumu la wanajeshi wetu.Isitoshe, tunaelewa pia kuwa kuvijenga upya vikosi vya ulinzi vya Afghanistan, kutawezekana tu iwapo wanajeshi wetu wa na Polisi wetu wa Ujerumani wakichukua jukumu hilo.Nakariri tena kwamba,shina la juhudi zetu huko ni kuwahudumia raia."

Katika kuutunga mkakati wake mpya kwa Afghanistan,Marekani imepima na kuona fursa za kuweza kuiimarisha zaidi na kuijenga upya Afghanistan, zimeongezeka .Anasisitiza mjumbe maalumu wa Ujerumani Mutzelburg:

"Hadi sasa ,kimsuingi, wamarekani wamekuwa wakiimarisha Afghanistan kwa mkono mmoja-ule wa shoto.Mkono wapili ule wa kulia ulikuwa nchini Irak.Sasa lakini ,wamarekani wana hisi kuijenga upya na kuimarisha Afghanistan , ni jukumu lake la kwanza na inapaswa kuligharimia kifedha."

Bw.Mutzelburg,anathamini mno pia juhudi za Marekani za kujipatia marafiki na washirika wapya. Anasema ndio hadi sasa mchango wa washirika ukikaribishwa,lakini kulikuwapo tofauti kubwa katika kuitathmini hali ya mambo,shabaha ya kufuatwa na yepi kuwekwa mwantzo.

Isitoshe, mchango wa kijeshi inaotoa Ujerumani nchini Afghanistan una shabaha ya kuleta masharti bora ya kuweza kuijenga upya nchi hii.Mchango wa Marekani ukiangalia ujenzi wa taasisi za kiraia na huduma zake ni jambo la pembezoni na ikitanguliza shughuli zake za kijeshi.

Fikra hizo hivi sasa , zimebadilika mno -kwa muujibu wasemavyo mabingwa.Msimamo wa sasa wa Marekani, unalingana na ule wa Ujerumani.

Zaidi ya hapo, suluhisho la mgogoro wa Afghanistan leo linatafutwa kimkoa pia.Ni hapo ambapo jirani Pakistan , inatoa mchango wake mkubwa -asema mjumbe maalumu wa Ujerumani.....

Kwahivyo, Jumuiya ya Kimataifa itafaulu tu kuimarisha Afghanistan,ikiwa pia nchini Pakistan, vikundi vyenye na itikadi kali, vikikandamizwa-wasema mabingwa.

Badiliko la mkakati wa Marekani, limechangia kwahivyo, kwa Jamii nzima ya kiamataifa kuvuta kamba nayo pamoja .

Mtayarishaji :Prema Martin

Mhaririri: Mohammed Abdul-Rahman