1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Afghanistan itaweza kujilinda yenyewe kuanzia mwaka 2015?

Admin.WagnerD8 Oktoba 2012

Serikali ya Afghanistan inaweza kuanguka baada vikosi vya NATO kuondoka nchini humo 2014, hasa iwapo uchaguzi wa urais utahusisha udanganyifu, Kundi la Kimataifa linaloshughulikia mizozo (ICG) limesema.

https://p.dw.com/p/16MS8
Ni moja ya silaha za kivita za vikosi vya Jeshi la NATO nchini Afghanistan
Ni moja ya silaha za kivita za vikosi vya Jeshi la NATO nchini AfghanistanPicha: REUTERS/Stuart Phillips/U.S. Navy/Handout

Serikali ya Afghanistan inaweza kuanguka baada vikosi vya NATO kuondoka nchini humo mwaka 2014, hasa iwapo zoezi la uchaguzi litahusisha vitendo vya udanganyifu, Kundi la Kimataifa linaloshughulikia mizozo limesema katika taarifa yake.

Mchambuzi wa ngazi ya juu wa kundi hilo nchini Afghanistan, Candace Rondeaux amesema kuna mashaka makubwa kwamba serikali ya Afghanistan inaweza kuporomoka kwa kuondoka kwa majeshi ya Jeshi la NATO. Ameongeza kusema kuwa fursa ya marekebi &sho nayo inayoyoma kwa haraka.

Afghanistan: The Long, Hard Road to the 2014 Transition"

Taarifa hiyo iliyopewa jina Afghanistan: Barabara ndefu na ngumu hadi kipindi cha mpito kuelekea 2014, inasema taifa hilo linaelekea kuwa na uchaguzi uliojaa visa vya udanganyifu, baada ya kuendesha uchaguzi wa urais na wabunge wa mwaka 2009 na 2010 uliogubikwa na vurugu za kila aina.

Askari wa ulinzi wakiwa katika doria mjini Kabul
Askari wa ulinzi wakiwa katika doria mjini KabulPicha: picture-alliance/dpa

Iwapo machafuko yatatokea tena katika uchaguzi wa urais ujao Afghanistan, matumaini finyu yaliyopo ya amani kurejea tena nchini humo yatapotea kabisa, baada ya serikali hiyo kuchukua jukumu zima la ulinzi wake kutoka kwa vikosi vya Jeshi la NATO, vinavyoongozwa na Marekani. Hayo ni kwa mujibu wa uchambuzi uliofanywa na Kundi la Kimataifa linaloshughulikia mizozo ICG, lenye makao yake makuu mjini Brussels, Ubelgiji.

Ushirika huo ambao umepigana vita kwa miezi 11 sasa dhidi ya wanamgambo wa Taliban, unapunguza idadi ya askari wake kutoka 130,000 ambapo mpaka kufikia mwishoni mwa mwaka 2014 askari wote wanatakiwa kuwa wamekwisharejea nyumbani.

Kwa mujibu wa maelezo ya mchambuzi huyo Rondeaux, polisi wamelemewa na aghalab hushambuliwa na wapiganaji hao wa Taliban. Rais Hamid Karzai na bunge lake wameshindwa pia kuchukua hatua thabiti za kuandaa zoezi la uchaguzi lililo huru na la haki.

Watoto kama huwa huathirika na mashambulizi yanayofanywa na wapiganaji wa Kundi la Taliban
Watoto kama huwa huathirika na mashambulizi yanayofanywa na wapiganaji wa Kundi la TalibanPicha: dapd

Karzai anachojali ni kuwa na ushawishi tu uongozini: Candace Rondoeaux

Aidha, mchambuzi huyu anasema Karzai anaonekana kujali zaidi kuendeleza nguvu yake badala ya kuhakikisha Afghanistan inakuwa na mfumo imara wa siasa na utulivu. Ingawaje amesema bayana kuwa ataondoka madarakani mwaka miaka miwili ijayo, kama katiba ya nchi inavyodai, lakini kuna hofu kuwa anaweza kusababisha hila katika uchaguzi huo ili kumweka mtu wake wa karibu madarakani, bila shaka mmoja wa kaka zake.

Wakati huohuo, mawaziri wa ulinzi wa NATO watapitisha mkakati mpana wa mafunzo yatakayoendeshwa Afghanistan baada ya kuondoka kwa majeshi ya NATO, wakati ambapo machafuko yanaendelea kutokea nchini humo na kuzua maswali mengi juu ya usalama wa nchi hiyo.

Mawaziri hao watakaokutana kesho na Jumatano mjini Brussels, yalipo makao makuu ya umoja huo, wanatazamiwa kuidhinisha mpango huo unaolenga kutoa mafunzo, ushauri na msaada kwa majeshi ya ulinzi ya Afghanistan, yatakayobeba jukumu la kulinda nchi hiyo kuanzia mwihoni mwa mwaka 2014.

Mwandishi: Ndovie, Pendo Paul\ AFP\ RTRE

Mhariri:Mohammed Abdul-Rahman