1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

ADEN : Waislamu wa Somali wataka mazungumzo na Ethiopia

17 Desemba 2006
https://p.dw.com/p/CCik

Uongozi wenye nguvu wa Kiislam nchini Somalia inaonekana kuwa tayari kufunguwa milango ya mazungumzo na nchi jirani ya Ethiopia ili kuepusha vita na serikali dhaifu ya Somali inayoungwa mkono na Ethiopia.

Afisa wa nganzi ya juu wa Muungano wa Mahkama za Kiislam nchini Somalia Sheikh Sharrif Ahmed amesema muungano huo uko tayari kuwa na mazungumzo na Ethiopia ambayo ina wanajeshi wake nchini Somalia kuihami serikali ya mpito ya nchi hiyo.

Wakati huo huo Ahmed na spika wa bunge la Somalia wametangaza makubaliano ya kuwarudisha tena kwenye meza ya mazungumzo uungozi wa Kiislam na serikali baada ya mazungumzo hayo kusambaratika mwezi uliopita.

Hata hivyo matumaini ya kufanyika kwa mazungumzo hayo hayako dhahiri kwa vile uungozi wa Kiislam umeipa Ethiopia hadi Jumanne kundoka nchini Somalia au kuwa tayari kwa vita na serikali ya Somali imesema fursa ya kuwa na mazungumzo imefungwa.