1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

ADDIS ABABA:Waziri mkuu wa Ethiopia aulaumu upinzani nchini humo

6 Mei 2005
https://p.dw.com/p/CFG5

Waziri mkuu wa Ethiopia Meles Zenawi ameonya kwamba ushindi wa upinzani katika uchaguzi unaotarajiwa kufanyika tarehe 15 mwezi huu huenda ukasababisha mauaji sawa na yale yaliyotokea nchini Rwanda akiwalaumu wapinzani wake kwa kujaribu kuchochea uhasama wa kikabila nchini humo.

Chama kinachotawala nchini humo cha Ethiopian Peoples Revolutionary Demokratic Front kinatarajiwa kushinda muhula wa tatu wa kipindi cha miaka mitano lakini upinzani unazidisha kampeini dhidi ya chama hicho.

Meles amesema wapinzani wake wanaendeleza siasa za chuki kwa waethiopia sawa na jinsi lilivyofanya kundi la wahutu wa Intarahamwe nchini Rwanda na kusababisha mauaji ya halaiki dhidi ya watsutsi mwaka 1994.

Vyama vya Upinzani nchini Ethiopia vinavyafanya kampeini ya kukiondoa katiba kukiondoa kipengele katika katiba ya nchi hiyo kinachoruhusu kujitenga kwa jimbo lolote kati ya majimbo tisa ya nchi hiyo kifungu ambacho waziri mkuu Zenawi anasema kitaleta mgawanyiko iwapo kitaondolewa.