1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

ADDIS ABABA: Waziri mkuu wa Ethiopia Meles Zenawi apiga marufuku Maandamano nchini humo

16 Mei 2005
https://p.dw.com/p/CFD8

Waziri mkuu wa Ethiopia Meles Zenawi amepiga marufuku maandamano yoyote nchini humo kwa kipindi cha mwezi mmoja kufuatia uchaguzi mkuu wa hapo jana.

Akizungumza kupitia Televisheni ya Taifa Zenawi alisema vikosi vya usalama mjini Adis vitawepokea amri moja kwa moja kutoka kwake.

Katika uchaguzi huo wa hapo jana idadi kubwa ya waethiopia ilijitokeza huku Zenawi na chama chake cha Ethiopian Peoples Revolutionary Demokratic Front akitarajiwa kushinda uchaguzi huo.

Hata hivyo upinzani umetishia kuyapinga matokeo ya uchaguzi huo katika misingi ya udanganyifu na kutolewa vitisho.

Zenawi ameliongoza taifa la Ethiopia tangu mwaka 1991 baada ya kuundoa madarakani uongozi wa kidekteta.