1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

ADDIS ABABA: Watu wanne wauwawa katika mapambano na polisi.

5 Novemba 2005
https://p.dw.com/p/CELj

Kiasi watu wanne wameuwawa nchini Ethiopia katika mapambano kati ya polisi na waandamanaji. Waandamanaji wanadai kuachiwa huru kwa wanachama wenzao wa upinzani ambao wanashikiliwa na polisi.

Katika muda wa wiki moja iliyopita , watu kadha wameuwawa na mamia wamejeruhiwa katika mapambano kama hayo katika madai ya udanganyifu katika uchaguzi mkuu wa taifa uliofanyika hapo May mwaka huu.

Katika hatua nyingine, umoja wa Afrika umeeleza wasi wasi wake juu ya hatua ya upelekaji wa majeshi katika maeneo yanayotenganisha nchi mbili hizo za Ethiopia na Eritrea.

Maafisa wa umoja wa mataifa wiki hii wamesema kuwa wanahofia mapigano mengine ya mpakani huenda yakatokea kati ya nchi hizo mbili.