1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Addis Ababa. Watu tisa wauwawa kwa bomu la kutupwa kwa mkono.

25 Julai 2005
https://p.dw.com/p/CEqr

Maafisa nchini Ethiopia wanasema kuwa watu kiasi tisa wameuwawa na wengine 20 wamejeruhiwa katika shambulio la bomu la kutupwa kwa mkono mashariki mwa nchi hiyo.

Watu ambao hawajulikani wameripotiwa kutupa mabomu matatu ya mkono katika makao ya maafisa wa serikali , baa na hoteli katika miji mitatu tofauti katika jimbo wanamoishi Wasomali nchini Ethiopia.

Maafisa wamesema kuwa ni mapema mno kusema iwapo shambulio hilo linahusiana na uchaguzi unaotarajiwa kufanyika katika jimbo hilo hivi karibuni.

Viti 23 vya bunge vitagombaniwa mwezi ujao, baada ya kuamuriwa kufanyika uchaguzi tena kufuatia madai ya udanganyifu katika uchaguzi mkuu wa hapo May 15.