ADDIS ABABA Watu 8 wauwawa katika machafuko nchini Ethiopia
8 Juni 2005Watu wasiopungua tisa wameuwawa mjini Addis nchini Ethiopia na wengine zaidi ya 100 wakajeruhiwa mapema leo wakati askari wa kuzima fujo walipokabiliana na waandamanaji wanaoyapinga matokeo ya uchaguzi wa mwezi uliopita nchini humo. Duru za hospitali ya Black Lion zinasema watu watatu kati yao waliuwawa kwa kupigwa risasi vichwani.
Wizara ya habari na utangazaji nchini humo imefutilia mbali vibali vya waandishi habari watano wa mashirika ya kigeni ya radio Deutsche Welle na sauti ya Marekani, wanaoripoti matukio yanayoendelea nchini humo kinyume cha sheria.
Waandishi hao wameonywa watachukuliwa hatua kisheria iwapo watapatikana wakiendelea na shughuli zao nchini humo. Serikali pia imesema itawachukulia hatua waandishi habari kama hao siku za usoni wataopatikana wakiripoti habari za uongo na kuegemea upande mmoja wanapotoa habari.