1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

ADDIS ABABA: Watalii wametoweka kaskazini-mashariki ya Ethiopia

3 Machi 2007
https://p.dw.com/p/CCMx

Serikali ya Ethiopia inaamini kuwa hadi watu 20 wa kigeni wametekwa nyara walipokuwa wakisafiri katika eneo la ndani nchini humo ambako waasi wanapigania kujitenga.Makundi mawili ya watalii waliotoweka siku ya Jumatano wakati wa kuzuru eneo kame la Afar kaskazini-mashariki ya Ethiopia.Kundi moja ni la kama watalii 10 wa Kifaransa na jingine ni raia wa nchi tofauti. Waziri wa masuala ya nje wa Uingereza,Margaret Beckett amethibitisha kwamba wafanyakazi 5 wa ubalozi wa Uingereza mjini Addis Ababa,ni miongoni mwa watu hao wasiojulikana walipo.Ripoti zisizothibitishwa zimesema,kundi mojawapo liliwasiliana na kampuni lao la utalii kwa njia ya simu ya satalaiti.Katika miaka ya hivi karibuni,eneo la Afar limeshuhudia vitendo vingi vya utekaji nyara.