1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

ADDIS ABABA: Watalii wa Kifaransa hawakuwa hatarini

4 Machi 2007
https://p.dw.com/p/CCMQ

Juhudi za kuwasaka Waingereza 5 waliotoweka nchini Ethiopia zinaendelea.Polisi wa Ethiopia wamesema,watalii hao walitekwa nyara pamoja na madreva na wakalimani 13 wa Kiethiopia katika eneo la ndani la Afar,kaskazini-mashariki ya mji mkuu Addis Ababa.Wafanyakazi wa ubalozi wa Uingereza ni miongoni mwa watu hao.Wakati huo huo ripoti zinasema wanajeshi wa Ethiopia waliokuwa wakipiga doria karibu na mpaka wa Eritrea, wamewapata Waethiopia 5 waliokuwa katika kundi la Waethiopia 13.Haijulikani ikiwa walitoroka au waliachiliwa huru.Leo hii waziri wa habari wa Eritrea,Ali Abdu alikanusha madai ya Ethiopia kuwa wanamgambo wa Kieritrea ndio walioliteka nyara kundi hilo siku ya Alkhamisi.Kwa upande mwingine,kundi la watalii wa Kifaransa lililotoweka tangu Alkhamisi,limewasili mji mkuu wa Afar,Mekele na wamesema,hawakutekwa nyara na wala hawakuwa hatarini.