1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

ADDIS ABABA: Wapinzani 38 waachiliwa huru Ethiopia

21 Julai 2007
https://p.dw.com/p/CBgb

Serikali ya Ethiopia imeachilia huru kundi la wapinzani 38,baada ya kukosolewa na jumuiya ya kimataifa kwa sababu ya kutoa adhabu kali.Mahakama Kuu ya Ethiopia,siku ya Jumatatu ilitoa kifungo cha maisha kwa washtakiwa 35 na wengine 8 walipewa kifungo cha jela,kuanzia miezi 18 hadi miaka 18.Watu hao 43 walishtakiwa kuwa walitaka kuipindua serikali,kufuatia uchaguzi wa mwaka 2005 uliozusha mabishano na machafuko makubwa.Waziri Mkuu wa Ethiopia,Meles Zenawi amesema,washtakiwa walioachiwa huru watapewa haki zao za kikatiba.Hata hivyo lakini,alisisitiza kuwa watarejeshwa jela ikiwa hawatoheshimu katiba na utawala wa kisheria.