ADDIS ABABA Wapiga kura tena nchini Ethiopia
22 Agosti 2005Wananchi wa Ethiopia wamepiga kura ya marudio katika majimbo kadhaa, kufuatia malalamiko juu ya uchaguzi mkuu uliofanyika nchini humo mnamo mwezi mei.
Matokeo ya uchaguzi huo yamepingwa na vyama vya upinzani kutokana na tuhuma kwamba udangayifu ulifanyika.
Ghasia zilitokea na watu 40 waliofanya maandamano kupinga matokeo hayo waliuawa baada ya kushambuliwa na polisi.
Watu pia walipiga kura katika jimbo la Somali, miezi mitatu baada ya sehemu zingine za nchi kufanya hivyo.
Hatahivyo kulikuwa na malalamiko juu ya kukawizwa kwa wapiga kura kutokana na foleni ndefu.
Matokeo ya kura hiyo ya jana hayataathiri viti vya wabunge wa sasa.
Viti vyote vya jimbo la Somali, vinakaliwa na wabunge wanaofungamana na waziri mkuu Meles Zenawi.
.