1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Addis Ababa. Wapatanishi kwenda Sudan.

21 Mei 2007
https://p.dw.com/p/CBzz

Wapatanishi kutoka umoja wa Afrika watakwenda nchini Sudan , Chad na jamhuri ya Afrika ya kati kujaribu kupunguza hali ya wasi wasi inayotokana na mzozo wa Darfur.

Taarifa ya umoja wa Afrika imesema jana Jumapili kuwa wajumbe sita watazuru wiki hii nchini Sudan pamoja na nchi jirani za Chad na jamhuri ya Afrika ya kati ili kupata tadhmini ya kina juu ya hali katika eneo hilo.

Ujumbe huo pia unajukumu la kuangalia vikwazo vinavyokwamisha utekelezaji wa makubaliano yaliyotiwa saini na Chad na Sudan ili kuweza kutoa mapendekezo ambayo yatasaidia kuleta suluhisho la kudumu katika matatizo ya eneo hilo.

Sudan na Chad zinashutumiana kwa kila upande kuwasaidia waasi wa nchi nyingine huku kukiwa na hofu miongoni mwa jumuiya ya kimataifa kuwa mzozo wa Darfur utaingia nchini Chad na kusababisha vita katika eneo lote.