1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

ADDIS ABABA : Wanajeshi 150 wakimbilia Eritrea

10 Agosti 2006
https://p.dw.com/p/CDMl

Zaidi ya wanajeshi 150 wa Ethiopia wameliasi jeshi kufuatia generali mmoja wa jeshi kukimbilia Eritrea wakati hali ya mvutano kati ya nchi hizo mbili ikiendelea kutokota kutokana na mzozo wa mpaka.

Kwa mujibu wa afisa wa kulinda amani wa Umoja wa Mataifa wanajeshi hao walikimbilia Eritrea wakati wa usiku hapo Ijumaane.Afisa huyo ambaye yuko mjini Addis Ababa na kikosi cha Kulinda Amani cha Umoja wa Mataifa amesema hawajuwi sababu za kuasi kwa wanajeshi hao lakini inaonekana kwamba huo ni uasi wa idadi kubwa kabisa ya wanajeshi wa Ethiopia kuwahi kushuhudiwa.

Ethiopia ilitangaza kuasi kwa Brigedia Generali Kemal Geltu ambaye alikuwa kamanda wa kikosi cha jeshi cha 18 kwenye televisheni ya taifa hapo Jumanne lakini haikusema kwamba kuna wanajeshi wengine waliohusika.