ADDIS ABABA Wanafunzi na polisi walumbana
8 Juni 2005Matangazo
Polisi mjini Addis Ababa wamo katika kibarua kigumu cha kukabiliana na wanafunzi wanao andamana katika vurugu za uchaguzi nchini Ethiopia.
Maandamano hayo yamo katika siku yake ya pili, visa vya wanfunzi kuwarushia mawe polisi vimeripotiwa.
Katika vurugu hizo mtu mmoja ameuwawa na zaidi ya watu 500 wamekamatwa.
Wanafunzi na wafuasi wa vyama vya upinzani mjini Addis Ababa wanapinga matokeo ya uchaguzi ambapo wanadai kuwa matokeo hayo ya ubunge ya tarehe 15 mwezi Mai yalikuwa na udanganyifu mkubwa.