ADDIS ABABA: Wanadiplomasia wamekamatwa Ethiopia
20 Oktoba 2006Matangazo
Nchini Ethiopia wanadiplomasia 2 kutoka Ulaya, wamekamatwa na kutangazwa kuwa ni watu wasiotakiwa nchini humo.Wizara ya mambo ya kigeni ya Ethiopia mjini Addis Ababa imesema wanadiplomasia hao watafukuzwa kutoka nchi hiyo. Inasemekana kuwa wanadiplomasia hao,walijaribu kuwasaidia wahalifu kwenda Kenya.