1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Addis Ababa. Waliotekwa nyara waachiwa huru.

14 Machi 2007
https://p.dw.com/p/CCJI

Watu watano raia wa mataifa ya Ulaya ambao walikuwa wametekwa nyara nchini Ethiopia kiasi cha wiki mbili zilizopita wameachiliwa huru. Waziri wa mambo ya kigeni wa Uingereza Margaret Beckett amewaambia waandishi wa habari mjini London kuwa Waingereza watatu, mwanamke mmoja raia wa Uingereza mwenye asili ya Italia na mwanamke mwingine raia wa Ufaransa wameachiliwa huru nchini Eritrea na wamechukuliwa na ubalizi wa Uingereza mjini Asmara.

Watu wote hao watano ni wanadiplomasia wa Kiingereza ama jamaa zao.

Hata hivyo , waziri Beckett amesema kuwa raia wanane wa Ethiopia ambao nao walitekwa nyara pamoja na raia hao wa mataifa ya Ulaya bado hawajaachiwa.

Mateka hao walikuwa katika matembezi ya kitalii katika jimbo la Afar lililoko kaskazini mashariki ya Ethiopia ambako walikamatwa na watu wenye silaha March mosi.