1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

ADDIS ABABA : Wafadhili watowa wito wa utulivu

21 Mei 2005
https://p.dw.com/p/CFBd

Wafadhili wa kigeni wa Ethiopia leo wametowa wito wa kuwepo utulivu wakati matokeo ya awali ya uchaguzi wa bunge wa wiki iliyopita yakionyesha upinzani ukiongeza karibu maradufu viti vyake bungeni.

Huku kukiwa na mzozo mkali juu ya kuaminika kwa uchaguzi huo wa Jumapili na malalamiko ya kuchelewa kutolewa kwa matokeo mabalozi kutoka nchi 21 za mataifa ya kigeni wameitaka serikali ya Ethiopia,upinzani na wananchi kuwa na subira na kuheshimu dhima ya bodi ya uchaguzi ya taifa katika kuhesabu na kutowa matokeo.

Wakati kura za majimbo 33 ya uchaguzi zikiwa zimekamilika kuhesabiwa Bodi ya Uchaguzi ya Taifa ya Ethiopia imesema viti 25 vya bunge vimechukuliwa na vyama vikuu viwili vya upinzani na vinane vimechukuliwa na chama tawala cha EPRDF