1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

ADDIS ABABA: Waasi wadai wameua wanajeshi 270

5 Novemba 2007
https://p.dw.com/p/C79v

Nchini Ethiopia waasi wa Chama cha Ukombozi wa Kitaifa wa Ogaden wamesema,wamewaua zaidi ya wanajeshi 270 katika mapamabano mapya yaliyozuka katika jimbo la Ogaden.Vikosi vya serikali katika eneo hilo la machafuko vinajaribu kukomesha harakati za waasi.Kwa mujibu wa waasi,baadhi kubwa ya wanajeshi waliripuliwa ndani ya magari yao.Serikali haikusema cho chote kuhusu madai hayo na hakuna thibitisho huru,kwa sababu eneo hilo ni marufuku kwa waandishi wa habari na pia ni shida kwa wafanyakazi wa mashirika ya misaada kufika katika eneo hilo.