ADDIS ABABA: Viongozi na wafuasi wa upinzani wazuiliwa kambini
12 Juni 2005Matangazo
Chama kikuu cha upinzani nchini Ethiopia,kimetoa wito wa kuachiliwa huru kiongozi wake aliezuiliwa kutoka nje ya nyumba yake kufuatia machafuko yaliotokea kuhusika na uchaguzi wa hivi karibuni.Wapinzani na wanafunzi wamelalamika kuwa uchaguzi wa mwezi uliopita ulifanyiwa udanganyiifu.Kwa mujibu wa Muungano wa Umoja na Demokrasia,wanachama na wafuasi wa upinzani kwa mamia,wamekamatwa na wamepelekwa katika kambi za majeshi.Jumatano iliyopita watu 26 waliuawa,baada ya polisi kuwafyetulia risasi wafanya maandamano katika mji mkuu Addis Ababa.