ADDIS ABABA: Vikosi vya Umoja wa Afrika vitaongezwa Darfur
30 Aprili 2005Matangazo
Umoja wa Afrika umeamaua kuongeza maradufu idadi ya wanajeshi wa kulinda amani katika jimbo la Darfur,magharibi mwa Sudan ifikapo mwezi wa Septemba.Hadi hapo watakuwepo wanajeshi na polisi 7,700 kuhakikisha kuwa mapigano yamesitishwa na pia kuwazuia wanamgambo waliokuwa wakiwashambulia wakazi wa vijijini tangu miaka miwili.Umoja wa Afrika umepitisha uamuzi huo,baada ya Umoja wa Kujihami wa Nchi za Magharibi-NATO kuahidi kuwa utatoa misaada kama vile ya uchukuzi.