ADDIS ABABA: Vikosi vya Kiafrika kuondoka Darfur
6 Septemba 2006Matangazo
Umoja wa Afrika umethibitisha kuwa muda wa vikosi vyake vya amani katika jimbo la mgogoro la Darfur nchini Sudan hautorefushwa baada ya kumalizika mwisho wa mwezi huu wa Septemba.Ujumbe huo sasa uchukuliwe na Umoja wa Mataifa,kwani tume ya Umoja wa Afrika una upungufu wa pesa na ufundi na haukuweza kufanikiwa.Wiki iliyopita Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa lilipitisha azimio kuchukua uongozi wa vikosi vya amani vya Umoja wa Afrika na kuongeza idadi ya wanajeshi hadi 20,000.Sudan lakini imepinga azimio hilo na badala yake imetuma wanajeshi wake kaskazini mwa Darfur.