1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

ADDIS ABABA: Upinzani hakuridhika na uchaguzi

24 Mei 2005
https://p.dw.com/p/CFAu

Chama kikuu cha upinzani nchini Ethiopia kimetishia kuwa hakitohudhuria kikao kijao cha bunge ikiwa malalamiko yake kwamba ulikwepo udanganyifu mkubwa wa kura katika uchaguzi mkuu wa wiki iliyopita,hayatotanzuliwa.“Muungano wa Umoja na Demokrasia“ umesema,ushahidi uliotolewa na chama hicho kuhusu ukiukaji wa utaratibu lazima ufanyiwe uchunguzi na tume iliyo huru.Chama tawala cha EPRDF kwa upande wake pia kimeutuhumu upande wa upinzani kuwa umefanya udanganyifu wa kura.Waangalizi wa kimataifa wamesifu chaguzi zilizofanywa tarehe 15 mwezi Mei na wameshauri yafanywe majadiliano kuumaliza ugomvi wa kisiasa.Matokeo ya mwisho ya chaguzi za bunge yanatarajiwa kutangazwa tarehe 8 Juni.