1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

ADDIS ABABA: Umoja wa Afrika walaani shambulio dhidi ya waziri mkuu wa Somalia

7 Novemba 2005
https://p.dw.com/p/CEKn

Umoja wa Afrika na umoja wa mataifa umelilaani shambulio dhidi ya waziri mkuu wa Somali, Ali Mohammed Gedi, lililofanywa mwishoni mwa juma. Bwana Gedi, aliponea chupuchupu katika jaribio la kutaka kumuua alipoutembela mji wa Mogadishu.

Walinzi wake watano waliuwawa na maofisa wengine 12 wakajeruhiwa vibaya wakati msafara wake wa magari uliposhambuliwa. Msemaji wa serikali amesema mripuko uliotokea ulisababishwa na bomu la kutegwa ardhini.

Mjumbe maalumu wa umoja wa mataifa nchini Somalia, Francois Fall, amesema shambulio hilo linazisambaratisha juhudi za kutafuta amani na kuyazika matumaini ya kumalizika kwa hali ya wasiwasi ambayo imekuwa ikiendelea kwa miaka 14.

Msemaji wa halmashauri ya umoja wa Afrika mjini Addis Ababa Ethiopia amewatolea mwito wasomali wakome kutumia machafuko badala yake watafakari njia za kuijenga upya nchi yao.