ADDIS ABABA : Umoja wa Afrika kuwa na mkutano wa dharura juu ya Dafur
10 Oktoba 2005Matangazo
Baraza la Amani na Usalama la Umoja wa Afrika linatazamiwa kukutana kwa dharura leo hii kujadili shughuli zake huko Dafur kufuatia mauaji na kutekwa nyara kwa walinda amani wa umoja huo.
Adam Thiam msemaji wa Mkuu wa Umoja wa Afrika Alpha Konare amesema nchi wanachama wa baraza hilo zitatakiwa kulaani vitendo hivyo na kutafita njia za kuvikomesha.
Adam alikuwa akizungumza kufuatia matukio ya hivi karibuni huko Dafur ambapo waasi hapo Jumamosi wamewauwa wanajeshi wawili wa kulinda amani wa AU kutoka Nigeria na makandarasi wawili na kuwateka nyara walinda amani wengine 38 kabla ya kuwaachilia leo hii.