ADDIS ABABA : Umoja wa Afrika kuongeza maradufu wanajeshi wake Dafur
30 Aprili 2005Matangazo
Umoja wa Afrika umeamuwa kuongeza maradufu wanajeshi wa kulinda amani katika jimbo la Dafur nchini Sudan ifikapo mwezi wa Septemba.
Kufikia wakati huo wanajeshi na polisi wa Umoja wa Afrika 7,700 wengi wao wakitokea Kenya, Nigeria na Rwanda watakuwa wamewekwa kusimamia usitishaji lege lege wa mapigano pamoja na kuwazuwiya wanamgambo ambao kwa miaka mwili wamekuwa wakiwashambulia wanakijiji.
Uamuzi huo wa Umoja wa Afrika unafuatia ahadi ya Umoja wa Kujihami wa Mataifa ya Magharibi NATO kwamba itausaidia umoja huo na misaada kama vile ya uchukuzi.