ADDIS ABABA: Uhaba wa chakula nchini Ethiopia
23 Februari 2005Matangazo
Umoja wa Matifa umeonya kwamba huenda Ethiopia ikakumbwa na uhaba wa chakula hivi karibuni. Watu milioni mbili na laki nne wanahitaji msaada wa dharura wa chakula nchini humo.
Kufikia sasa ni asilimia 11 pekee ya chakula cha msaada kinachohitajika kufikia marchi kilichotolewa na wafadhili.Tani elfu 39 za chakula bado zinahitajika. Kwa mujibu wa Umoja wa Matifa idadi ya watu wanaohitaji chakula inatarajiwa kuongezeka na kufikia milioni mbili na laki tisa mwezi marchi na kufikia milioni tatu na laki moja ifikiapo mwezi April.Umoja wa Mataifa umesema mapigano ya kikabila kufuatia mzozo wa kudhibiti wilaya ya Meisso kilomita 500 mashariki mwa mji wa Addis yamesababisha
ongezeko la watu wanaohitaji msaada nchini humo.