ADDIS ABABA: Tume ya maafisa wa Uingereza imewasili Ethiopia
3 Machi 2007Matangazo
Maafisa wa Uingereza wamewasili katika mji mkuu wa Ethiopia,Addis Ababa kujaribu kupata uhuru wa kundi la watalii wa kizungu.Inadhaniwa kuwa watalii hao wametekwa nyara na waasi katika eneo la ndani la Afar,lililo kaskazini-mashariki ya Ethiopia.Siku ya Ijumaa,waziri wa masuala ya nje wa Uingereza,Margaret Beckett alithibitisha kuwa wafanyakazi watano wa ubalozi wa Uingereza mjini Addis Ababa,ni miongoni mwa watu wanaodhaniwa kuwa wametekwa nyara.Ripoti zinasema,watalii wa Kifaransa na Waethiopia 13 pia hawajulikani walipo.Katika miaka ya hivi karibuni,eneo la Afar limeshuhudia vitendo vingi vya utekaji nyara.