ADDIS ABABA. Rais Mkapa amaliza ziara yake nchini Ethiopia
31 Agosti 2005Ethiopia na Tanzania zimetia saini mkataba wa ushirikiano katika biashara na utalii.
Mkataba huo umetiwa saini katika siku ya mwisho ya ziara ya rais wa Tanzania Benjamin Mkapa nchini Ethiopia.
Mapema rais Mkapa aliwahutubia wana diplomasia wa Umoja wa nchi za Afrika katika makao makuu ya umoja huo juu ya changamoto zinazo likumba bara la Afrika katika biashara ya kimataifa.
Amezitaka nchi za Afrika kutafuta mbinu za kujikuza kiviwanda badala ya kutegemea uuzaji wa bidhaa zao katika nchi za Ulaya na Marekani.
Katika hotuba yake ya kuiaga kamisheni ya umoja wa Afrika rais Mkapa alimnukuu mwandishi maarufu wa Ujerumani Goethe kwa kusema “Tukiwaamini watu jinsi walivyo ndivyo tunavyo wapa nguvu walizo nazo’’.
Rais Mkapa alisema anataraji bara la Afrika litajizatiti kulinda hadhi yake katika siku za usoni.