ADDIS ABABA: Rais Mbeki ajiuzulu kama mpatanishi wa mzozo wa Ivory Coast
18 Oktoba 2006Matangazo
Rais Thabo Mbeki wa Afrika Kusini amejiuzulu kama mpatinishi katika mzozo wa kisiasa wa Ivory Coast.
Mwenyekiti wa Umoja wa Afrika, rais Denis Sassou Nguesso, alisema rais Mbeki kwa hiari yake aliwasilisha pendekezo la kujiondoa kutoka kwa jukumu hilo.
Msemaji wa rais Mbeki, Mukoni Ratshitanga, amesema uamuzi huo umetokana na kuchaguliwa kwa Afrika Kusini kuwa mwanachama wa muda wa baraza la usalama la Umoja wa Mataifa, hatua ambayo ambayo amesema itaitatiza kazi yake ya upatinishi.
Rais Dennis Sassou Ngweso amependekezwa achukue mahala pa rais Mbeki.