1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

ADDIS ABABA: Pendekezo la Ufaransa lakataliwa na Sudan

12 Juni 2007
https://p.dw.com/p/CBsW

Serikali ya Sudan imeukataa mpango wa Ufaransa wa kutaka kuitisha mkutano wa kimataifa baadae mwezi huu,mjini Paris kuujadili mgogoro wa Darfur. Waziri wa nje wa Ufaransa,Bernard Kouchner ameambiwa na waziri mwenzake wa Sudan,Lam Akol kuwa “wakati huu si muafaka”.Maafisa wa Umoja wa Mataifa,Umoja wa Afrika na wa Sudan wanakutana Addis Ababa mji mkuu wa Ethiopia.Viongozi hao wanaujadili mpango wa kupeleka Darfur wanajeshi 23,000 wa Umoja wa Mataifa na Umoja wa Afrika kulinda amani katika jimbo hilo la mapigano.Sudan inataka vikosi hivyo viwe chini ya uongozi wa Umoja wa Afrika,wakati Umoja wa Mataifa ukitaka kuwa na mfumo wake wa uongozi.Watu 200,000 wameuawa na kiasi ya wakazi milioni 2.5 wamepoteza makazi yao,tangu mapigano kuzuka katika jimbo la Darfur mwaka 2003.