1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

ADDIS ABABA: Mwito wa wagombea haki za binadamu haukuitikiwa

25 Juni 2005
https://p.dw.com/p/CF0S

Umoja wa Afrika umeukataa mwito uliotolewa na nchi za magharibi na makundi ya kimataifa yanayotetea haki za binadamu,kuwa Umoja huo uchukue hatua ya kusitisha kampeni ya serikali ya Zimbabwe ya kubomoa nyumba.Msemaji wa Umoja wa Afrika amesema,Umoja huo una matatizo makubwa zaidi ya kushughulikiwa.Inakadiriwa kuwa hadi watu 300,000 hawana mahala pa kuishi,tangu kuanzishwa kwa kampeni ya serikali ya Harare majuma sita ya nyuma.Polisi nchini Zimbabwe,wamekuwa wakiwafukuza watu majumbani mwao na wamebomoa nyumba katika mji mkuu Harare na miji mingine.Rais Robert Mugabe wa Zimbabwe anasema,hatua ya kuzibomoa nyumba hizo ni sehemu ya kampeni ya kupambana na uhalifu.Lakini wakosoaji wanasema,lengo la kitendo hicho ni kuwaadhibu wale wanaowaunga mkono,wapinzani wa kisiasa wa rais Mugabe.