ADDIS ABABA: Mwito wa kukomesha mateso jimbo la Darfur
19 Novemba 2006Serikali ya Sudan na wanamgambo wa Janjaweed wametuhumiwa na Umoja wa nchi za Afrika kuwa wamefanya mashambulio mapya katika jimbo la Darfur.Umoja wa Afrika ulio na wanajeshi 7,000 katika jimbo hilo la mgogoro,magharibi mwa Sudan,umesema mashambulio yaliofanywa hivi karibuni kutoka angani na ardhini,yameua na kujeruhi watu darzeni kadhaa.Maafisa wa Umoja wa Afrika wamesema mashambulio hayo ni ukiukaji dhahiri wa makubaliano ya usalama ya mpito kuhusu Darfur.Mkuu wa huduma za kiutu wa Umoja wa Mataifa,Jan Egeland alipozungumza mjini Khartoum baada ya ripoti ya tuhuma hizo kuchomoza alitoa mwito kwa serikali ya Sudan ishirikiane na Umoja wa Mataifa ili kukomesha mateso katika jimbo la Darfur.Serikali ya Khartoum hadi hivi sasa haikutoa jawabu lake.