1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

ADDIS ABABA: Mkuu wa Benki ya Dunia ziarani Afrika

11 Julai 2006
https://p.dw.com/p/CG8Y

Mkuu wa Benki Kuu ya Dunia,Paul Wolfowitz ameanza ziara yake barani Afrika,kabla ya kufunguliwa mkutano wa kilele wa madola tajiri yaliyoendelea kiviwanda duniani.Wolfowitz aliwasili Ethiopia Jumatatu usiku kwa ziara yake ya pili barani Afrika,tangu kushika wadhifa wa rais wa Benki Kuu ya Dunia mwaka moja wa nyuma.Ataizuru Tanzania kabla ya kwenda St.Petersburg nchini Urussi kuhudhuria mkutano wa kilele utakaofanywa kuanzia tarehe 15 hadi 17 mwezi huu.Amesema,kwenye mkutano huo,atawahimiza viongozi kuyasaidia madola ya Kiafrika yaliyo masikini kabisa kujitoa kwenye janga la umasikini na kuwa na maendeleo,ili kizazi kijacho kiwe na maisha yaliyo bora.