Addis Ababa. Matokeo ya uchaguzi yatolewa rasmi.
6 Septemba 2005Matangazo
Ethiopia imetoa jana Jumatatu matokeo ya mwisho ya uchaguzi mkuu na kuthibitisha chama tawala cha waziri mkuu wa sasa Meles Zenawi na washirika wake kimeshinda uchaguzi huo ulioingia dosari baada ya kulalamikiwa na upande wa upinzani kuwa kulikuwa na udanganyifu.
Baada ya karibu miezi mitatu ya kuhesabu kura , matokeo ya mwanzo yaliyotolewa August 9 yalikipa chama cha Bwana Zenawi cha Ethiopian Peoples Revolutionary Democratic Front ushindi.
Vyama vya upinzani vimekataa kukubali matokeo hayo.