ADDIS ABABA: Mafuriko yachelewesha misaada
19 Agosti 2006Matangazo
Wasaidizi kusini-magharibi mwa Ethiopia wanajitahidi kwa shida kuwaokoa watu walionasa juu ya mapaa na kwenye miti kwa sababu ya mafuriko makubwa yaliyotokea.Wasaidizi hao wamesema,hali mbaya ya hewa na uharibifu uliotokea unachelewesha zaidi juhudi zao za misaada.Inaaminiwa kuwa hadi watu 8,000 wamezungukwa na mafuriko na kama 900 wameripotiwa kuwa wamefariki au hawajulikani walipo.Vile vile kiasi ya watu 75,000 wamepoteza makazi yao katika mafuriko hayo.Mvua kubwa zilizonyesha zimesababisha mafuriko sehemu mbali mbali nchini Ethiopia.