1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Addis Ababa. Leo ni siku ya uchaguzi nchini Ethiopia.

15 Mei 2005
https://p.dw.com/p/CFDR

Leo ni siku ya upigaji kura katika uchaguzi mkuu nchini Ethiopia ambao unatarajiwa kwa kiasi kikubwa kuwa waziri mkuu Meles Zanawi ataibuka na ushindi kwa kipindi kingine cha awamu ya tatu.

Vyama 35 vitashiriki katika uchaguzi huo kugombea viti katika bunge la nchi hiyo, ambalo chama tawala cha Ethiopia Peoples Revolutionary Democratic Front EPRDF kina viti vingi.

Vyama vya upinzani vinakishutumu chama tawala kwa kushindwa kuondoa ukiritimba wa serikali katika umilikaji wa ardhi, ambao vinasema unasababisha hali mbaya ya upungufu wa chakula nchini humo. Pia wanamshutumu waziri mkuu Meles Zenawi kwa kushindwa kupiga hatua katika kuiondoa nchi hiyo katika umasikini, wakisema kuwa miito ya kuipatia nchi hiyo misaada ya chakula ya mara kwa mara , inaipa sura ya taifa la omba omba.

Hata hivyo kinyume na uchaguzi uliofanyika mwa