1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

ADDIS ABABA : Konare ataka wanajeshi watumwe Somalia

26 Januari 2007
https://p.dw.com/p/CCXm

Mkuu wa Umoja wa Afrika amezitaka nchi wanachama wa umoja huo hapo jana kuwatowa wanajeshi wao kwa haraka kwa ajili ya shughuli za kulinda amani nchini Somalia kabla ya kufanyika kwa mkutano wa viongozi wa naazi ya juu wiki ijayo.

Umoja wa Afrika unajaribu kukusanya kikosi cha wanajeshi 8,000 kuzuwiya uwezekano wa kuwepo pengo la usalama katika nchi hiyo ya Pembe ya Afrika wakati wanajeshi wa Ethiopia wakijiandaa kuondoka.

Alpha Omar Konare amezitaka nchi zote kuonyesha mshikamano zaidi kwa kutowa wanajeshi,fedha na misaada ya vitu.

Masuala kadhaa tata yatakuwa juu kwenye agenda katika Mkutano wa Viongozi wa Umoja wa Afrika Au hapo tarehe 29 na 30 mwezi wa Januari ambapo viongozi wa Kiafrika pamoja na Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon watajadili shughuli za kulinda amani nchini Somalia pamoja na shauku ya Sudan kutaka kuwa Mwenyekiti wa Umoja wa Afrika.