ADDIS ABABA: Kiongozi wa zamani wa Ethiopia, Mengistu Haile Mariam, ahukumiwa adhabu ya kifungo cha maisha gerezani.
11 Januari 2007Matangazo
Rais wa zamani wa Ethiopia, Mengistu Haile Mariam, amehukumiwa adhabu ya kifungo cha maisha gerezani kwa mauaji ya halaiki.
Rais huyo wa zamani alipatikana na hatia mwezi uliopita baada ya kesi iliyoendeshwa kwa muda wa miaka kumi na miwili.
Mengistu Haile Mariam kwa sasa hivi anaishi uhamishoni nchini Zimbabwe.
Kiongozi huyo wa zamani alikuwa ameshtakiwa kwa kuwaua maelfu ya watu wakati wa utawala wake wa muda wa miaka kumi na saba tangu mwaka elfu moja mia tisa na sabini na nne alipompindua mfalme Haile Selassie.
Hata hivyo, serikali ya Zimbabwe imesema haitamkabidhi Mengistu Haile Mariam kwa Ethiopia.