Addis Ababa. Kansela awasili kwa ziara barani Afrika.
4 Oktoba 2007Matangazo
Kansela wa Ujerumani Angela Merkel amewasili nchini Ethiopia usiku wa leo akianza ziara yake ya mataifa ya Afrika ambayo itamchukua hadi Afrika kusini na Liberia.
Merkel , ambaye anafanya ziara hiyo akiwa na waziri wa ushirikiano na maendeleo Heidemarie Wieczorek-Zeul, wabunge na viongozi wa makampuni kadha, amelakiwa kwa heshima za kijeshi na atakuwa na mazungumzo na viongozi wa kisiasa nchini humo baadaye leo.
Ziara hiyo ya kwanza kusini mwa jangwa la Sahara katika bara la Afrika, inatarajiwa kulenga katika haki za binadamu, ukimwi, ushirikiano wa kiuchumi na mzozo wa kisiasa nchini Zimbabwe.