ADDIS ABABA: Kampeni za uchaguzi nchini Ethiopia
7 Mei 2005Matangazo
Waziri Mkuu wa Ethiopia Meles Zenawi hii leo ameanza kufanya kampeni ya uchaguzi utakaofanywa tarehe 15 Mei nchini humo.Chama chake tawala EPRDF kinatazamiwa kushinda kwa mara ya tatu kwa mfululizo na hivyo kuingoza nchi kwa miaka mitano mingine.Lakini vyama vitano vikuu vya upinzani vimeweka kando tofauti zake na vimeunda muungano imara kabisa kumpa Meles changamoto kali.Meles ametoa muito kwa Waethiopia kutowapigia kura wapinzani akisema wanaendeleza fikra za mgawanyo wa kikabila.Vyama vya upinzani vinapigania kukitoa kifungu kimoja kwenye katiba.Kwa mujibu wa kifungu hicho jimbo lolote lile miongoni mwa majimbo tisa ya kikabila yanayounda taifa la Ethiopia,yana haki ya kujitenga.Wapinzani wanasema kifungu hicho kinadhoofisha umoja.