ADDIS ABABA: Joaquim Chissano ateuliwa mpatanishi wa umoja wa Afrika katika mzozo nchini Zimbabwe
11 Agosti 2005Matangazo
Umoja wa Afrika umemteua rais wa zamani wa Msumbuji Joaquim Chissano kuwa mpatanishi katika mazungumzo ya kisiasa nchini Zimbabwe. Mwenyekiti wa umoja wa Afrika, rais Olusegun Obasanjo wa Nigeria, amemtaka Chissano kuongoza mazungumzo kati ya chama tawala nchini Zimbabwe ZANU PF cha rais Robert Mugabe na chama cha upinzani cha Movement for Democratic Change, kinachongozwa na Morgan Changirai.
Hatua hiyo inafuatia kukosolewa kwa umoja wa Afrika kwa kushindwa kuchukua hatua yoyote juu ya uvunjaji wa makaazi ya walalahoi. Umoja wa mataifa unasema ukatili huo wa serikali ya Zimbabwe ulisababisha watu elfu 700 kupoteza makaazi au kazi zao.