ADDIS ABABA: Idadi ya vifo vyaongezeka
17 Agosti 2006Matangazo
Idadi ya vifo vilivyosababishwa na mafuriko nchini Ethiopia imeongezeka kufikia 1,000, baada ya maiti nyengine 170 kupatikana.
Mamia ya raia bado hawajulikani waliko huku wengine takriban elfu 30 wakiwa wameachwa bila makao baada ya nyumba zao kuharibiwa.
Maeneo yaliyoathiriwa zaidi yako katika eneo la kusini ambako mto Omo ulifufirika na kuvizamisha vijiji yapata 14.
Umoja wa Mataifa umeitolea mwito jamii ya kimataifa ipeleke misaada ya kiutu nchini Ethiopia.