ADDIS ABABA: Hofu ya vita kuzuka katika Pembe ya Afrika
30 Novemba 2006Matangazo
Bunge la Ethiopia limetoa idhini kwa serikali kuchukua hatua yo yote ile iliyo halali dhidi ya wanaharakati wa Kiislamu wenye nguvu katika nchi jirani Somalia.Uamuzi huo wa bunge umezidisha hofu kuwa vita huenda vikaripuka katika kanda hiyo.Bunge la Ethiopia lilipitisha uamuzi huo saa chache tu baada ya wanamgambo wanaounga mkono Mahakama za Kiislamu kudai kuwa wamefanya mashambnulio mapya dhidi ya vikosi vya Ethiopia nje ya mji wa Baidoa wenye makao ya serikali ya mpito ya Somalia na ikiwa ni siku moja baada ya wapiganaji hao kuituhumu Ethiopia kuwa imeshambulia mji wanaoudhibiti.